Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Naibu Meya na Diwani wa Levolosi wapokea kichapo

$
0
0

02052010506

Na Mahmoud Ahmad Arusha

Naibu Meya wa jiji la Arusha Prosper Msofe na diwani wa kata ya Levolosi Ephatar Nanyaro wamepokea kichapo kutoka kwa mgambo wa halmashauri ya jiji la Arusha kwenye yadi ya halmashauri hiyo iliyopo kwenye kata ya Levolosi jijini hapa.

Kadhia hiyo iliyowakuta madiwani hao waliokuwa wakifuatilia malalamiko ya wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo (Almaarufu machinga) waliokuwa wakilalamikia kunyanganywa mali zao na mgambo hao  na kupekea vichapo kila wanapokamatwa hali iliyowalazimu viongozi hao kwenda kushuhudia kwa macho yao yale yaliokuwa ya kisemwa na wafanyabiashara hao.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kwenye kikao hicho cha muda Naibu meya wa halmashauri ya jiji la Arusha Prosper Msofe alisema kuwa walipofika eneo hilo walikuta wafanyabiashara na mafundi nguo waliokuwa wakidai vifaa na mali zao na ndipo walioanza kuhoji na kujikuta wakipokea kichapo hicho.

Alisema kuwa ameumia sehemu za kwenye mbavu na mguuni maeneo ambayo alipigwa na marungu na mgambo wa jiji na mwenzake diwani wa kata ya Levolosi kuumia kwenye mdomo na kupatiwa matibabu kwenye zahanati ya Ngarenaro.

Hata hivyo ndani ya ofisi za halmashauri hiyo mafundi wanaoshona nguo kwenye vibaraza mbalimbali jijini hapa walikusanyika ilikupata tamko ama waendelee kufanya shughuli zao au wasiendelee kwani wamekuwa wakipata usumbufu kutoka kwa mgambo wa jiji na kujikuta wakinyang’anywa mashine zao na vifaa vyao vya kazi kila wanapofungua licha ya kupewa kibali cha kuendelea na shughuli zao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa mafundi ambaye ni katibu wa umoja wa mafundi nguo jijini Arusha, Ester Lyimo alisema kuwa wapo hapo ilikupewa kibali walichoahidiwa kwani kila ahadi wanayopewa imekuwa ikivunjwa na mgambo hao wa halmashauri ya jiji kwa kuwachukulia vifaa vyao na kuvipeleka depot.

Lyimo pia alisema kuwa wamekuwa akidai kulipia vifaa vyao kwa faini ya tsh 50000 bila ya kupewa risiti na unapohoji wamakuwa wakipokea kichapo ndani ya depot hiyo huku akihoji kuwa je gwantanamo bay imehamia hapa Arusha hata hivyo hadi gazeti hili lilipoondoka maeneo hayo liliwaacha hapo bila ya viongozi husika kutoa majibu kwao.

Hata hivyo zoezi zima la operesheni ya kuliweka jiji safi kwa kuwaondoa wamachinga wanaofanyabiashara holela opembezoni mwa barabara na kwenye vibaraza vya nyumba zilizopo katikati ya jiji limesitishwa hadi hapo taarifa zitakapotolewa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles