Wafanyakazi wa TOTAL kwenye picha ya pamoja.
Nishati ni moja ya nguzo muhimu katika kupunguza umasikini na kukuza uchumi. Ukuaji wa Teknolojia ya mawasiliano, elimu, viwanda, kilimo na miundombinu ya maji katika manispaa, vyote vinahitaji nishati ya uhakika, inayotosheleza na yenye gharama nafuu.
Karibia bilioni mbili ya watu duniani hawajaunganishwa na gridi ya taifa na hawapati huduma ya umeme. Mamilioni ya nyumba Africa katika maeneo ya vijijini ambapo umeme haupatikani, au upatikana kwa bei ya juu wanatumia njia mbadala za nishati. Wengi wao wanategemea mkaa, kuni na mafuta ya taa.
Hata hivyo, matumizi ya mkaa, kuni na mafuta ya taa, yana hararibu rasilimali, na upatikanaji wake unapungua kulinganisha na ongezeka la idadi ya watu pamoja na mahitaji yao. Kwa sasa, manilioni ya watu wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa nishati iliyo bora na isiyo ya gharama.
Nishati ya jua kama nishati mbadala isiyochafua mazingira ni ya bure, na mataifa ya Kiafirka yanaweza kulinda wananchi wao kimazingira na kuleta maendeleo yao ya kiuchumi kwa kutumia vyanzo vya nishati mbadala.
Nchi nyingi za Kiafrika zinapata mwanga wa jua kwa wastani wa siku 325 kwa mwaka, hii inasababisha nishati ya jua kuweza kupatikana katika eneo lolote Africa bila kutumia gridi ya taifa ambayo ni gharama kubwa.
Zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji ya nishati ya umeme nchini Tanzania, yanafikiwa na kutumia mkaa, kuni na mafuta ya taa. Watanzania wamekua wakiendelea kutumia vyanzo vya nishati vya kizamani na visivyo vya uhakika, wakazi wa hali ya kawaida ya maisha wamekua wakitumia hadi 35% ya rasilimali kufikia mahitaji yao ya nishati kwa kutumia kuni na mkaa. Nyumba nyingi zinatumia majiko yasio na ufanisi yanayopunguza matumizi makubwa ya nishati, ambayo yanasababisha uchafuzi wa mazingira ikiwemo ndani ya nyumba na hali ya hewa iwazungukayo. Hii inasababisha matumizi makubwa ya pesa na muda mwingi wanatumia kutafuta hii nishati mbadala yaani kuni na Mkaa, ambayo kwa muda mrefu inawaathiri wanawake na watoto.
Juhudi za kuendeleza miundombinu ya teknolojia ya nishati mbadala Tanzania kwa miongo iliyopita ilikosa usimamizi bora. Kwa sasa, shirika lisilo la kiserikali, Tanzania Renewable Energy Association (TAREA), iko mstari wa mbele kuchangia kukuza nishati mbadala endelevu kwa Tanzania kwa kutoa mafunzo kwa jamii, kuongeza uelewa, na kuendeleza sera, , kufanya, utafiti, kutoa programu za kujitolea, huduma za ushauri na huduma zitolewazo na washiriki,
TAREA na mashirika mengine wanatumia mikakati tofauti katika sekta ya nishati mbadala kwa kulenga kuendeleza upatikanaji wa nishati mbadala safi na nafuu katika nyumba za kuishi na biashara ndogo na za kati kupitia mbinu endelevu za kimasoko.
TOTAL kupitia program yake ya TATS, imeunga mkono mashirika mengine katika kusaidia ukuaji wa bidhaa zenye ubunifu, ambazo ni salama kwa afya na mazingira.
Lengo la TOTAL kuingia kwenye sekta hii si la kibiashara au kiushindani, bali ni kusaidia kuendeleza uwezekano wa soko lenye faida. Bidhaa za AWANGO zinatazamia kuleta faida kwa wateja na wafanya biashara, taa za nishati ya jua pamoja na chaja, zitaleta manufaa kwa watu wa hali ya chini kwa kutoa nishati nafuu inayoendana na ubora wa kimataifa. Bidhaa hizi zitapatikana katika vituo vya mafuta vya TOTAL Tanzania nzima, na kwa watu wenye kipato cha chini katika maeneo ya vijijini watapata bidhaa hizi kupitia mpango maalum. Total itashirikiana na mitandao mbalimbali ya usambazaji ili bidhaa hii iwafikie watu huku wakiwa na nia ya kufikia lengo lao la kuwaelimisha wakazi wa vijijini juu ya bidhaa tofauti na ufanyaji kazi wake na kuwaelimisha juu uwezekano wa nafasi ya biashara.
AWANGO toka TOTAL inatazamia kugusa jamii kwa njia mbalimbali, na haitizamii tu ukuaji wa maendeleo ya kijamii bali kuwawezesha watu kibiashara. AWANGO ina mpango wa kuwasajili wafanyabiashara wasambazaji katika maeneo ya vijijini, na mkakati huu utawezesha njia itakayoruhusu kufanya biashara yenye mafanikio kulingana na uwezo wao wa kuwafikia wateja wao. Kwa kusaidia kuanza biashara TOTAL inashirikiana na mashirika ya kijamii kutoa mikopo kwa watu, inayowaruhusu kununua bidhaa hii.
AWANGO inawaahidi sio tu kuwaletea mwanga bali kuwaongezea kipato watanzania wengi. Ikisukumwa na ahadi ya TOTAL kupitia Total Access to Solar (TATS), AWANGO inalenga kuwafikia Watanzania milioni 5 kufikia 2015.