Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma Machi 6, 2014 baada ya Bunge hilo kusitihwa kwa muda kufuatia Sitofahamu iliyotokea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Halima Mdee akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa kwa muda mjini Dodoma Machi 6, 2014 kufuatia sintofahamu iliyokea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa muda Machi 6,2014 kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).